Breaking News

REA YASAMBAZA MAJIKO YANAYOTUMIA UMEME UNITI MOJA KWA SAA

 


Wellu Mtaki, Dodoma .

Wakala wa Nishati Vijijini (REA)  wameanza kusambaza majiko ya umeme yenye matumizi nafuu, likiwemo jiko linalotumia uniti moja tu ya umeme kwa saa moja.


Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Utawala wa  wakala wa nishati vijijiji , Renatus Msangira   wakati akizungumza na waandishi  wa habari jijini Dodoma       katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma huku akisema kuwa juhudi za Rais Samia zimewezesha kufikiwa kwa vijiji vyote nchini kupatiwa huduma ya umeme  pamoja na kuelekeza nguvu zake katika kusambaza huduma  hadi kwenye vitongoji.


Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi wa REA, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa maono yake. Kupitia dira yake, tumefanikisha kupeleka umeme katika vijiji vyote nchini, na sasa tumeanza awamu mpya ya kuhakikisha vitongoji vyote navyo vinaunganishwa na huduma hiyo muhimu,” amesema Msangira.

Aidha, alieleza kuwa REA inaunga mkono kwa vitendo kaulimbiu ya Rais Samia inayosisitiza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa afya na mazingira bora. Alisema