Breaking News

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA WATANZANIA WOTE WAPATE HAKI ZAO - WAZIRI MKUU MAJALIWA

Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mhe. Kassim Majaliwa

Na Hawa Ismail, Dar es Salaam

Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe 16- 06-2025 amezindua kamvpeni ya ya uzinduzi wa msaada wa kisheria ya mama Samia katika viwanja vya maturubai mkoani Dar es Salaam itakayofanyika ndani ya siku kumi.

Aidha kauli mbiu ya kampeni hiyo ni msaada wa kisheria kwa haki, usawa, amani na maendeleo hivyo kupitia kauli mbiu hiyo itasaidia kutakua change changamoto kwa usimamizi wa sheria kokote ulipo nchini.

"Kupitia kampeni hii ya msaada wa kisheria ya mama Samia itasaidia kuwafikia watu wote katika wilaya zote na vijiji vyote vya mkoa wa Dar es Salaam itasaidia kila mwananchi atapata amani, haki bila ubaguzi wowote" amesema Majaliwa

Aidha kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Albert Chalamila amesema kwamba kupitia kampeni hii itasaidia kutatua migogoro ya kisheria na kuaacha kutumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kuvunja sheria.

"Watu wachache wazusha kupitia mitandao ya kijamii mimi kama mkuu wa mkoa sipokei  vitisho napokea ushauri" amesema chalamila

Hata hivyo waziri wa katiba na sheria Mhe. Damas Ndumbaro amesema kwamba lengo la kampeni hii ni kuelimisha, kutoa msaada wa kisheria na kufuta 4r za mama samia.

"Kupitia kampeni hii tutakuwa na maridhiano, tutafuata usuluhisho, tutakuwa na ustahimilivu na kujenga upya misaada ya kisheria hivyo katika utekelezaji wa 4r za mama Samia" amesema Ndumbaro

Mwakilishi UN- WOMEN TANZANIA bi. Hodan Addou nao wameunga mkono kampeni ya msaada wa kisheria ya mama samia

Aidha bi. Addou alisema kwamba kupitia kampeni hii itasaidia sana kutetea haki za wanawake katika Jamii wanazoishi hivyo itapelekea wanawake  kujumuika kwa pamoja katika jamii

Aidha Majaliwa alikabidhi vifaa vya kitechnolojia kwa jeshi la magereza ili kurahisisha msaada wa kisheria kwa jeshi la magereza.