Breaking News

Makada 38 wajitosa kugombea ubunge Wilaya ya Ilala

Na Heri Shaaban (CCM ILALA)

MAKADA 38 wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala wamejitosa katika kinyanganyiro cha  kuchukua fomu    kuomba ridhaa kugombea ubunge   kuomba kuongoza wa  wananchi katika majimbo manne Wilaya ya Ilala 

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa CCM wilaya ya Ilala Chief,Srilivester Yared,alisema zoezi la kutoa fomu  limeanza jana Juni 28 mpaka Julai 2 mwaka huu ambapo mwitikio umekuwa mkubwa kwa makada wa chama hicho.

"Makada wa chama cha Mapinduzi CCM nafasi ya ubunge waliojitokeza wilaya ya Ilala jimbo la Kivule,Jimbo la Ilala ,Jimbo la segerea jumla yake 38  kati ya Wagombea 38 wa Ubunge Jimbo la Ukonga wamejitokeza watatu,Jimbo la Ilala watano,Jimbo la Segerea watano,Jimbo la Kivule 22 "alisema Yared. 

Katibu Yared alisema kati ya wagombea 38 wa Ubunge wanawake saba na wanaume 31 wote wamechukua fomu katika kinyanganyiro hicho cha kura za maoni kwa ajili ya mchakato ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. 

Wakati huo huo alisema kwa upande waliochukua fomu nafasi ya Udiwani 134  kati ya wagombea 134   wanawake 29 na wanaume 105.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza la Wazazi Taifa Saady Kimji,amechukua fomu kwa kipindi cha awamu ya tatu kwa ajili ya kugombea nafasi Udiwani  kusubiri mchakato ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. 

Saady Kimji alisema amechukua fomu kwa ajili ya kupeperusha bendera ya chama kwani Ilala amefanya kazi kubwa za utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi kwa ajili ya kusimamia miradi ya Serikali vizuri ambapo katika uongozi wake ameweza kujenga shule za Sekondari shule za msingi ikiwemo shule ya Sekondari Mivinjeni,shule ya sekondari Kasuru ,shule ya English Medium Mzizima Ilala na vituo vya afya vya kisasa Bungoni  ambacho kilifunguliwa na Waziri wa Nishati Doto Buteko .

Aidha Kimji alisema m mambo makubwa mengine aliyoyafanya ametekeleza Ilani kwa kujenga barabara za kisasa 17 na sekta elimu kuongeza ufaulu  

Kwa upande wake Nyansika Getama, amechukua fomu ya Udiwani Kata Kivule Wilayani Ilala Mkoa Dar es Salaam kwa ajili kugombea nafasi ya Udiwani Kivule. 

Nyansika Getama ,alisema anagombea nafasi ya Udiwani    Kivule ili aweze kuendeleza utekelezaji wa Ilani kwani katika kata ya Kivule amefanya mambo makubwa ikiwemo sekta ya elimu,sekta ya afya na ujenzi wa kituo cha Polisi cha kisasa  kilichofunguliwa na kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Isimail Ally Ussi. 

Mgombea Ubunge jimbo la  Kivule Frolian Mkyanguzi Karugaba alisema yeye alikuwa Mwenezi wa CCM Tawi  Msongola pia ni Mshauri kwa ngazi ya mashirika.

 Frolian Mkyaguzi Karugaba alisema amejitosa kugombea ubunge jimbo la Kivule kutatua changamoto mbalimbali za jimbo hilo kwani dhamira ya Serikali kuondoa kero hivyo atakaposhinda ubunge atatatua kero za wananchi ambapo alisema ana uwezo mkubwa akishinda ubunge atasimamia uwezeshaji wananchi kiuchumi waweze kunufaika