KAMANDA MULIRO KUIMARISHA ULIZI NA USALAMA KATIKA MECHI YA YANGA NA SIMBA UWANJA WA MKAPA JUNI 25
Na Hawa Ismail
Kamanda wa polisi kanda maalum Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi, (SACP) Jumanne Muliro ametangaza ulinzi na usalama katika mchezo wa Simba na Yanga utakao chezwa tarehe 25 juni 2025 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam alisistiza swala la usalama wa raia na mali zao pamoja na barabara zote zitakazo kuwa zinaelekea kwenye mchezo huo zitalindwa kwa sababu kutakuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu.
" Hatutaruhusu mtu au kikundi cha watu kuingia na silaha isipokuwa askari wachache" amesema kamanda Muliro
Aidha Kamanda Muliro amesema kwamba mchezo wa Simba na Yanga ni mchezo unaopendwa na watu wengi hivyo haitoruhusiwa vitendo vya udhalilishaji, kukiuka utaratibu wa ujunjaji wa mila na desturi zetu
.jpeg)