Trump amwambia Putin amalize 'vita vya kijinga' nchini Ukraine au akabiliwe na vikwazo vipya
Marekani
Donald Trump ameonya kuwa ataiwekea Urusi ushuru wa juu na vikwazo zaidi iwapo Vladimir Putin atashindwa kumaliza vita nchini Ukraine.
Akiandika katika mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, alisema kuwa kushinikiza kutafuta suluhu la vita hivyo ni "kuipendelea sana" Urusi na rais wake.
Trump awali alisema kuwa atajadili suluhisho la uvamizi kamili wa Urusi uliozinduliwa mnamo Februari 2022, kwa siku moja.
Urusi bado haijajibu matamshi hayo, lakini maafisa waandamizi wamesema katika siku za hivi karibuni kwamba kuna fursa ndogo kwa Moscow kushughulika utawala mpya wa Marekani.
