Breaking News

DRC: Tunachokifahamu kuhusu utekaji wa M23 wa maeneo ya Kivu Kusini na Kaskazini

 



Maelezo ya picha,Vikosi vya serikali vinapambana na waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo..

DRC CONGO

Wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametangaza kwamba wamerejesha udhibiti kusini mwa eneo la Lubero, katika milima ya Sake na Nyiragongo, kwa kuwarudisha nyuma waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.

Vikosi vya jeshi la DRC, ambavyo vilisema kuwa "vita dhidi ya uchokozi wa Rwanda vinaendelea katika pande zote", hata hivyo vilisisitiza kuwa "adui amefapata mafanikio katika eneo la Bweremana katika Kivu ya Kaskazini na Minova katika Kivu Kusini".

Hatua ya M23 kuteka mji wa Minova, ambao ni muhimu wa kibiashara mashariki mwa DRC, kunawaweka waasi wa M23 chini ya kilomita 40 kutoka mji mkuu wa jimbo wa Goma, uliopo karibu na mpaka na Rwanda.

"Minova iko mikononi mwetu," Corneille Nangaa, kiongozi wa Congo River Alliance, - muungano unaojumuisha kundi la M23, aliliambia shirika la habari la Reuters.