Breaking News

Tanzania Kuanzisha Mafunzo ya Marubani Wenye Vigezo vya Kimataifa

 



Na Mwandishi wetu Dar es Salaam 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi, amesema Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kipo kwenye hatua ya mwisho ya kupata cheti kitakachowawezesha kutoa mafunzo ya marubani wenye vigezo vya kimataifa.

Akizungumza Oktoba 17, 2024, katika kongamano la kimataifa la uchukuzi jijini Dar es Salaam, Msangi alieleza kuwa chuo hicho kinatarajiwa kuzalisha marubani watakaokuwa na uwezo wa kurusha ndege kwa viwango vya kimataifa. Hii inafuatia maelekezo ya Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, ya kutumia ndege mbili mpya kwa ajili ya mafunzo.

Msangi alisisitiza kuwa Tanzania inakabiliwa na uhaba wa marubani wenye sifa za kimataifa, na hatua hiyo inalenga kuboresha sekta ya usafiri wa anga nchini.