Breaking News

MAONESHO YA MIFUGO NA MNADA - TCCS LIVESTOCK SHOW AND AUCTION EVENT KUFANYIKA JUNE 14-15 2024 UBENA ESTATE CHALINZE



Na mwandishi wetu 
Chama cha Wafanyabiashara wa Ng’ombe Tanzania TCCS kwa kushirikiana na Benki Ya Maendeleo Ya Kilimo 
Tanzania (TADB) pamoja na NMB tumeandaa Maonesho ya Kimataifa ya Mifugo na Mnada yatakayofanyika June 14 hadi Juni 16 katika Viwanja vya Highland Estates, Ubena Estate, Ubenazomozi, Wilaya ya Chalinze. 
Maonesho hayo ya siku tatu yatawaleta pamoja wafugaji wa kibiashara, wauzaji wa ng'ombe wa nyama na maziwa, Wafugaji wa mifugo mbalimbali wakulima, wapenzi wa burudani pamoja na wasambazaji wa vifaa na pembejeo zingine.

 Tunachukua fursa hii kuwakaribisha wadau wote wa Mifugo waje kushiriki nasi wasikose nafasi hii adhimu na ya kipekee kutangamana na wenzetu kutoka sekta yetu na nafasi ya kununua kutoka kwa wafugaji bora nchini! 
Fahamu kuwa Tanzania Commercial Cattle Society TCCS ni shirika lililosajiliwa ambalo linawaleta pamoja wafugaji ambao wana nia moja katika kuendeleza idadi kubwa ya minyororo imara ya thamani ya mifugo ya kitaifa. 
TCCS inalenga kukuza kilimo kwa kuandaa maonyesho kama haya kila mwaka, yafahamikayo kwa jina la TCCS Livestock Show and Auction.
 
Lengo letu ni Kuwawezesha wafugaji, wasindikaji na wadau wengine nchini Tanzania kushawishi sera za maendeleo na kukuza uzalishaji wa mifugo endelevu kwa njia ya kuwajengea uwezo na mitandao. 
Nia yetu ni kuwezesha Jukwaa Madhubuti la kitaifa la wafugaji wa kibiashara, wasindikaji na wadau wengine katika minyororo wa thamani ya mifugo kutambulika kwa lengo moja la kuendeleza sekta hii kwa 
Mbinu bora endelevu za kiuchumi na kimazingira. 
Tamasha hili la wafugaji lilianzishwa na kuchukua nafasi yake kwa mara ya kwanza mwaka 2022, mwaka 
huu tunatazamia liwe na uboreshwaji mkubwa ambapo Tumejipanga kutoa msadaa mkubwa ndani ya jamii 
ya wafugaji na watumiaji. Lakini tutahakikisha pia ni tamasha litakaloweka historia tutaelimisha na 
kuburudisha umma, lakini pia kusaidia wafugaji na wakulima, kuonyesha urithi wa Tanzania na kutoa elimu kupiia semina mbalimbali zitakazoendeshwa kwenye siku hizo tatu za Maonesho. 
Tunamshukuru sana Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuweka mazingira Bora,

 Rafiki na wezeshi kwenye kuhakikisha sekta hii inawakwamua wakulima na wafugaji kimaisha nchi nzima. Rais wetu Mama Samia wakati akihitimisha sherehe za Kilele Cha Maonesho ya kimataifa ya Kilimo Nanenane mwaka jana yaliyofanyika Uwanja John Mwakangale Mkoani Mbeya, 

tarehe 08.08.2023 alisema Serikali itaendelea kuweka mazingira Rafiki ili kuwezesha wakulima wakiwemo wafugaji kujikwamua kiuchumi na kutoa wito kwa Wakulima Nchini Kuongeza Tija na ubunifu katika  shughuliza KILIMO.



Na Sisi kama TCCS tunaamini katika jitihada zake, na tutaendelea kutoa ushirikiano wa kuhakikisha kuwa 
tunaunga mkono Juhudi zilizofanywa na serikali yake katika kuboresha sekta hii, ikiwa ni pamoja na 
kuanzishwa kwa Programu ya Miaka 8 ya kujenga kesho Bora ya Vijana ijulikanayo kama Building Better Tomorrow (BBT) inayolenga kuhamasisha Vijana kuingia katika kilimo, hii ni Pamoja na ufugaji, kufanya Kilimo Cha Kisasa, ufugaji kibiashara kwa lengo ya kujikwamua kiuchumi kwa wao wenyewe na Taifa kwa ujumla. 
Ni kwa hali hiyo tunayofuraha kualika vijana wengi na wafugaji wapya au wanaotamani kuingia katika 

Tasnia hii kushirikiana nasi, tukio limepangwa kufanyika tarehe 14 -16 Juni 2024 pale Chalinze, Pwani Morogoro. Tukio hili linatarajiwa kupata washiriki zaidi ya 300, kutoka kila kona ya Afrika. likihusiha nyama choma, vyakula mbalimbaii, maonyesho ya mifugo, mnada, elimu ya ufugaji, semina na warsha pamoja na michezo mbalimbali ya wakubwa na wadogo. 
Kauli mbiu yetu: 
Ni “kuja pamoja katika Kuhakikisha sekta yetu inakua na kuwa sekta endelevu ya kijamii, kiuchumi na kimazingira. Kwa kingereza ni Making sure our sector develops into a socially, economically and environmentally sustainable industry. 

Katika Ulimwengu unaokabiliwa na matishio ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi uzalishaji endelevu wa mifugo na ulaji wa vyakula vyenye virutubishi vingi, vinavyotokana na wanyama vina jukumu muhimu 
katika kufikia malengo yetu ya maendeleo na yakimilenia. 
Ufugaji endelevu wa uchumi unaoongozwa na kilimo ni Ushahidi unaonyesha kuwa sekta ya mifugo inakuza pato la taifa (GDP) kwa wastani wa asilimia 30 katika nchi za kipato cha chini na kati. 
Kaya za vijijini zinategemea sana mifugo, huku 60% hadi 80% ya kaya zinamiliki mifugo ili kujikimu kimaisha, na zinaweza kutumika kama njia ya kuweka akiba. Na tunajua kwamba kaya, hasa katika maeneo hatarishi, lazima ziwe na uelewa wakina wa masuala ya ufugaji. 

Katika mambo yatakayozungumzwa ni pamoja na umuhimu wa sekta hii kwa jamii ambapo Ushahidi unaonyesha kuwa ni 18% tu ya watoto wanaopata lishe tofauti ya kutosha katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati. 

Vyakula vya asili ya wanyama, kama vile maziwa na mayai, vina virutubishi muhimu ambavyo vina jukumu muhimu katika kutoa virutubishi vinavyohitajika kwa ukuaji na maendeleo mapema 
maishani. Hatimaye, mifugo pia ni rasilimali muhimu kwa kaya katika maeneo yenye matatizo ya mara kwa mara, ambapo tunalenga jitihada zetu za kuimarisha ustahimilivu na kusaidia familia kuondokana na umaskini, hata katika kukabiliana na mishtuko na matatizo, ikiwa ni pamoja na majanga ya hali ya hewa. 

Walakini, mifumo mingi ya mifugo haifanyi kazi kwa ufanisi na usalama wa chakula na usafi unaweza kuwa 
suala la kuangalia. Sekta hii inachangia takriban asilimia 14% ya uzalishaji wa gesi chafu duniani kila mwaka, 
ingawa sehemu kubwa ya hiyo hutolewa katika nchi zilizoendelea. athari za sekta ya mifugo katika 
mabadiliko ya hali ya hewa, ni muhimu kukumbuka kuwa ushahidi uliopo unaonyesha kuwa kukuza lishe na usalama wa chakula kwa mifumo endelevu ya chakula kwa kutumia utafiti wa maendeleo pamoja na mbinu za kuzingatia hali ya hewa kunaweza kuboresha ufanisi na kupunguza kasi ya uzalishaji. 
. Uwekezaji wa Feed the Future katika mbinu ya mifumo ya chakula, ambayo inajumuisha uzalishaji endelevu wa mifugo, itachochea ukuaji wa uchumi, kuboresha lishe. Nani anatarajiwa kuhudhuria katika Maonesho haya? 
Wafugaji, wanunuzi, wauza malisho ya mifugo, madaktari wa mifugo, wauza pembejeo, wauzaji wa madawa ya mifugo, wauzaji wa mashine mbalimbali, wapenzi wa burudani, wafanyabiashara mbalimbali, 

watoa huduma na watoa maamuzi katika sekta ya Kilimo kutoka nchi nzima, pia tutakuwa na semina na warsha mbalimbali. Tunawaalika watu wote pamoja na watoto kuja kujifunza kufurahi na kushiriki katika kupata au kukuza utaalam wao wa Usimamizi na ufugaji endelevu wa sekta ya kilimo, kukutana ana kwa ana na serikali kuu, kufahamu namna ya ufugaji bora wa mifugo kibiashara, kununua Bidhaa mbalimbali za mashambani na kuhitimisha mikataba na washika dau wa kilimo. 
Tukio hili la furaha linajumuisha vibanda vya chakula, Maonyesho, michezo ya watu wazima na watoto na 
burudani nyingine mbalimbali pamoja na; kutengeneza urafiki wa Wateja na kuongeza mauzo usambazaji, 
ushirikiano au mawakala, kukutana na wateja wa sasa ana kwa ana na watoa maamuzi. Ikiwa ni pamoja 
nakufikia wataalamu wakuu wa kilimo na kujenga uhusiano mpya na wanunuzi,. Tukio hilo litahitimishwa 
na sherehe za kufunga zitafanyika tarehe 16 June katika viwanja hivyo hivyo ambapo kamati ya maandalizi 
itawatunuku washiriki, wawezeshaji na wadhamini vyeti vya ushiriki 
Maonesho haya yamedhaminiwa na; 
Benki ya maendeleo ya kilimo tanzania TADB ambao ndio wadhamini wetu wakuu na hii inakuwa mara yao 
ya pili kudhamini maonyesho hayo, pamoja na NMB, wadhamini wengine ni pamoja na Farmbase, African 
Fibres, Mbogo Ranches, Shafa Agro, Chobo Investments na wengineo ambao tutaendelea kuwatambulisha 
kadri muda unavyozidi kwenda. 
Tunatoa shukran zetu za dhati kwa wadau mbalimbali wa kilimo wanaoendele kujitokeza na kuonyesha nia 
ya kushirikiana nasi, kwa kipekee kabisa tunashukuru vyombo vya Habari kwa mchango wao mkubwa 
katika hili.