Breaking News

KAMPUNI YA HQ TANZANIA YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU



Na Mwandishi wetu, Dodoma

Katika kuonesha moyo wa upendo na kujali jamii, Kampuni ya HQ Tanzania imetoa msaada wa vifaa tiba kwa watoto wenye ulemavu wanaolelewa katika Kituo cha SBHD Foundation.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mkurugenzi wa SBHD Foundation Suma Geofrey ametoa shukrani za dhati kwa Mkurugenzi wa HQ Tanzania kwa moyo wake wa kujitolea na mchango mkubwa unaogusa maisha ya watoto wenye mahitaji maalum.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuunga mkono na kushiriki katika huduma za kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kutimiza ndoto zao na kuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya taifa.

- Kila msaada una thamani. Kila mtoto ana ndoto. Tuungane kuwajengea kesho iliyo bora.