Breaking News

TTCL Yatumia Bilioni 1.6 Kununuwa Magari na Bajaji Kuimarisha Huduma za Mawasiliano

 

Na Mwandishi Wetu- Dar es Salaam 

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Moremi Marwa, amekabidhi rasmi magari 9 na bajaji 28 kwa Wakuu wa Idara na Vitengo ili kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya Shirika.

Makabidhiano hayo yamefanyika Makao Makuu tarehe 29 Aprili 2026, ambapo imeelezwa kuwa jumla ya shilingi bilioni 1.6 zimetumika kununua magari aina ya Toyota Hilux, na shilingi milioni 291.2 kwa ajili ya bajaji 28.

"Uwekezaji huu unatokana na faida ya mwaka wa fedha 2024/25 ambapo Shirika lilipata bilioni 22.98. Lengo ni kuimarisha huduma na miundombinu ya mawasiliano nchini," amesema Mkurugenzi Mkuu.

Vyombo hivyo vitatumika kusimamia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, kuendeleza mradi wa Faiba Mlangoni Kwako, pamoja na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

Shirika pia linatarajia kupokea magari mengine 5 mwishoni mwa Mei 2026 ili kuendelea kuboresha shughuli za masoko na mauzo.