MSTAHIKI MEYA AAHIDI MAENDELEO KWENYE UFUNGUZI WA BARAZA JIPYA JIJI LA DAR ES SALAAM
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo, amelitaka Baraza la Madiwani, chini ya Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mheshimiwa Nurdin Bilal Juma, kushirikiana kwa karibu na watendaji na wataalamu wa jiji huku akisisitiza kwamba umoja na mshikamano ndiyo nyenzo muhimu ya maendeleo katika Jiji la Dar es Salaam.
Kauli hiyo ameitoa Disemba 4 ,2025 alipokuwa akizungumza na Baraza la Madiwani pamoja na wananchi katika mkutano wa kwanza wa baraza hilo
Mheshimiwa Mpogolo pia ameahidi kutoa ushirikiano kwa baraza hilo ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika na wananchi wanapata huduma bora.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Halmashauri hiyo kwa kipindi menejimenti ilikuwa ikikasimu madaraka na baraza la madiwani.


