Breaking News

*Prof. Kitila Mkumbo na Benedictor waahidi Maendeleo ya Miundombinu na Huduma za Jamii Mburahati*


Mgombea ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Profesa Kitila Mkumbo, amepongeza ushirikiano wa wananchi wa Kata ya Mburahati katika kuchochea maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita. Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za udiwani za CCM katika kata hiyo, alisisitiza dhamira ya kuendeleza juhudi za kuboresha huduma za jamii na miundombinu.

Prof. Kitila alisema, "Tumekuwa tukishirikiana katika kuboresha elimu, ujenzi wa soko la Mburahati, barabara na vivuko. Ushirikiano huu ni msingi wa kuunda serikali imara ya kata na taifa kwa ujumla."

Alieleza kuwa endapo atachaguliwa tena, ataanza na miradi mitano ya kipaumbele kupitia bajeti ya mfuko wa jimbo, ikiwemo:

- Ujenzi wa barabara ya Madoto hadi Mburahati kwa kiwango cha lami, ambapo shilingi bilioni 2 zimetengwa.

- Mradi wa barabara ya Barafu hadi Magomeni kwa kushirikiana na UNDP, ambapo mkandarasi tayari amepatikana.

- Uboreshaji wa barabara za Tegemeo na Mama Telesa kwa kushirikiana na Diwani Benedictor Malange.

- Ufuatiliaji wa bajeti ya milioni 10 kwa ajili ya miradi ya kata.

- Kuimarisha huduma za afya, hususan magonjwa ya moyo na saratani, kwa kuleta madaktari bingwa.

Aidha, alieleza kuwa CCM imefanyia utafiti wa kina ilani yake ya uchaguzi, ikijumuisha vipengele 261 vya utekelezaji, ikiwemo:

- Elimu bure kutoka shule ya msingi hadi kidato cha sita.

- Bima ya afya kwa wote kupitia mpango wa Mama Samia Suluhu Hassan wenye thamani ya milioni 20.

Kwa upande wake, mgombea udiwani wa CCM katika kata ya Mburahati, Ndugu Benedictor Joseph Malange, aliahidi kusimamia utekelezaji wa miradi ya vivuko katika mitaa ya Nation House na Barafu, pamoja na:

- Kuboresha upatikanaji wa mikopo kwa vijana na wanawake kwa usawa.

- Kuboresha Zahanati ya Mburahati kuwa kituo cha afya chenye huduma za mama na mtoto.

- Kusimamia ujenzi wa uzio katika shule ya sekondari ya Mburahati na kuimarisha ufaulu kwa kushirikiana na walimu na wazazi.

Viongozi hao waliwahimiza wakazi wa Mburahati kujitokeza kwa wingi ifikapo Oktoba 29 kupiga kura kwa ajili ya kuichagua CCM, ili kuendeleza mkataba wa maendeleo unaolenga kuibadilisha Mburahati kuwa kata ya kisasa yenye miundombinu bora, huduma za afya za uhakika, na elimu yenye ubora.

Tusifanye makosa. Tuchague Mama Samia Suluhu Hassan kwa urais, Prof. Kitila Mkumbo kwa ubunge, na Ndugu Benedictor Malange kwa udiwani ili Mburahati isonge mbele."_ alisema Malange.