Elizabeth Michael: Vipodozi vya Lumina vimeipendezesha ngozi yangu
![]() |
| Elizabeth Michael (Lulu), akiteuliwa kuwa Brand Ambassador wa Lumina Skin, 13 Agosti 2025, Dar es Salaam |
Msanii wa filamu almaarufu Lulu aingia mkataba wa ubalozi na Lumina Skin.
Na Kelvin Kijo, Dar es Salaam
Msanii wa kuigiza nchini Elizabeth Michael (Lulu) ameingia mkataba wa kuwa Brand ambassador wa vipodozi vya kampuni ya Lumina Skin inayojihusisha na kutengeneza vipodozi mbalimbali kwa jinsia zote (unisex) ikiwamo Lumina Aqua Hydrating Sunscreen, glowing cream, facial cleanser, na Lumina body spray.
Balozi huyo mpya wa Lumina Skin amesema anaviamini vipodozi hivyo kuwa vinaipendezesha ngozi ya mwanamke na mwanamume. “nimevijaribu katika ngozi yangu nikapata matokeo mazuri, pia nimehakikisha vipodozi vya Lumina vimekubalika kwenye maabara ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).” Amesema Lulu.
Lulu ameongezea kuwa yeye ni mrembo na anajua vipodozi mbalimbali hivyo aliwaomba ajiridhishe kwanza jinsi wanavyoendesha mambo yao, ubora wa bidhaa zao kabla ya kukubali kuingia mkataba wa muda mrefu na Lumina (Lulu hakataja ni wa miaka mingapi).
Vipodozi vya Lumina vina ingredients za viwango sahihi zenye kulinda ngozi katika hali zote na vinavyofaa katika ngozi ya watumiaji wengi bila kuwachubua, na kwa kila kundi za uchumi, nchini na nje ya nchi. “muhimu bidhaa zetu zinataka muendelezo kuzitumia (consistency) ili kupata matokeo yaliyobora kwa ngozi yako.” amesisita Lulu.
Kwa upande wake Maneja Masoko wa Lumina, madam Osmunda Ndimbo hakusita kuweka wazi kwa ujasiri kuwa vipodozi vya Lumina havina kemikali zozote za kuchubua ngozi na ndio mana TBS wamezikubali ziwafikie watumiaji, Lumina ina mikakati ya kuongeza bidhaa nyingine kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya wateja wao.
Osmunda amesema kampuni imefungua milango kwa mawakala wa kuuza vipodozi vya Lumina Dar es Salaam na mikoani, “Makao makuu (HQ) yapo Mwenge Plaza na tunawakaribisha mawakala Tanzania nzima kushiriki faida na ubora wa bidhaa zetu.”
Nje na maswala ya vipodozi msanii Lulu amesema kuwa anataka kuendelea kuwa balozi wa bidhaa na huduma mbalimbali, mipango ya kujikita katika kujipanua kiuchumi, na kuwekeza katika mali zisizohamishika.
.png)
