DKT. BITEKO "UBUNGE NI KAZI YA WATU"
Na mwandishi wetu
Akizungumza mbele ya Wajumbe, Mbunge anayemaliza muda wake Dkt. Doto Biteko amesema kuwa amerudi kwao akiamini kwamba wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Wananchi wa Bukombe ndio wanatoa ridhaa kwa mgombea kupata wadhifa huo.
“Nawaambieni ukitaka kufanya kazi ya ubunge rudi kwa watu, maana hii kazi ya ni ya Watu nenda kawaone wenye kazi yao, ndio maana kila nikienda baada ya muda lazima nirudi, nilikuwa narudi kwa watu na mlivyokuwa wema kila ninaporudi mnanipokea vizuri nafarijika”.
Aidha, Dkt. Doto Mashaka Biteko amesema kuwa miaka mitano iliyopita ilikuwa miaka ya kazi iliyopambwa na ushirikiano wa kutosha miongoni mwa viongozi na wanaCCM jambo lililokiwezesha Chama Cha Mapinduzi kupata heshima kubwa na leo nimekuja kwenu kuwashukuru sana na kwa unyenyekevu mkubwa ninawaomba kura zenu za ndiyo.
“Mimi sitaweka mawakala katika vituo vya kupigia kura kwa sababu sina mashaka na nyinyi watu wema wa Bukombe bali mawakala wangu mtakuwa ninyi wananchi wenyewe wa Bukombe”.



