CCM YAZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO MKOA WA DAR ES SALAAM
Na Mwandishi wetu- Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu leo Agosti 31,2025 amefungua kampeni katika mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha katika uzinduzi huo wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Sokoine kata ya Azimio wilaya ya Temeke uliuzuliwa na madiwani wote wa mkoa mkoa wa Dar es Salaam Pamoja na wabunge wote wa mkoa wa Dar es Salaam.
Hata hivyo Abbas Mtemvu aliwatambulisha wabunge wote pamoja na kuwakabidhi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Uchaguzi ya Mwaka 2025.






