BRELA YASHANGAZA WAFANYABIASHARA NANENANE
Na. Wellu Mtaki
Katika kuhakikisha Kila mfanyabiashara ana rasimisha biashara yake hasa wakulima wanaolima kilimo Cha biashara, Wakala wa Usajili wa Leseni( BRELA) wamekuwepo kuwahudumia vyema wafanyabiashara Katika wiki ya maadhimisho ya wakulima ( nanenane).
Hayo amebainisha Afisa Usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Leseni( BRELA) Gabriel Kirangay wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungwa kwa maonesho ya nanenane ambayo yalifungwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan huku akieleza kuwa wanatoa leseni ya viwanda pamoja na kasajili viwanda vidogo.
Aidha amesema kuwa Licha ya maonesho hayo ya nanenane kufikia hitimisho lake bado wanaendelea kutoa huduma hivyo amewakaribisha Wananchi kuendelea kutembelea ofisi zao mbalimbali nchini Tanzania ili waendelee kujifunza zaidi.
Sambamba na hayo amewashukuru wakulima pamoja na wananchi ambao wamekuwa wakifika kwenye Banda lao na kupata huduma ikiwa pamoja na kupokea maoni .


