Breaking News

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MH. DAMAS NDUMBARO AMEIPONGEZA OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA

 


Na Hawa Ismail, Saba Saba

Waziri wa katiba na sheria Mhe. Damas Ndumbaro ameipongeza ofisi ya mwandishi mkuu wa sheria kwa kutafsiri sheria 300 kutoka kingereza kwenda kiswahili.

Ameyasema hayo  leo julai 11, 2025 wakati alipokuwa anatembelea banda la ofisi ya mwandishi mkuu wa sheria ( OCPD) katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye maonesho ya 49 ya biashara (Sabasaba). 

Aidha Mhe. Ndumbaro alisema kazi za ofisi ya OCPD ni inafanyia marekebisho ya sheria na  kutungwa kwa sheria ndogo.

"Katika mwaka huu wa fedha tumetenga bajeti ili kuweza kufasiri sheria 146 zilizobaki jumla zote ni 446 ziwe kwa lugha ya kiswahili ili watanzania waweze kuzielewa" alisema Mhe. Ndumbaro 

Awali ofisi ya mwandishi mkuu wa sheria  (OCPD) ipo chini ya wizara ya katiba na sheria  na pia inaunga mkono kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia.