Breaking News

RAIS WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA (TFF) ASHIRIKI MKUTANO WA KUJADILI SOKO KA PAMOJA LA FILAMU AFRIKA MASHARIKI NCHINI UGANDA

 



Na Mwandishi Wetu.

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) Rajab Amiry  ameshiriki Mkutano wa siku tatu nchini Uganda ambao ulikuwa mahususi kujadili kutengeneza Muungano wakua na soko la pamoja la Filamu Afrika Mashariki.

Akizungumza Juni 11,2025  mara baada ya kuwasili kutoka Nchini Uganda, Rais huyo wa Shirikisho la Filamu Tanzania amesema kwamba Mkutano huo ulikuwa na malengo ya kutengeneza muungano wa makubaliano ya zaidi ya nchi nane,kutangaza kazi za filamu kupitia App ya  Steam Afrika.

Aidha amesema kwamba kwenye mkutano huo wamejdili namna gani wanaweza kupata masoko makubwa ya kuuza Filamu,na pia baada ya kujadiliana na  kukubaliana kuona kuweke utaratibu mzuri ambao wameingia makubaliano(MOU) ambayo itasaidia filamu za Afrika kua katika sehemu mzuri. 

" Tunashukuru serikali ya Uganda ambayo ilikuwa sehemu ya dhamana,ya UNESCO kwa ajili ya kufadhili Tanzania kwa kutuamini kwa kuwepo bodi ya filamu kwa kuwakilisha , Zanzibar  ilikuwepo katika mkutano huo" Amesema Rajab

Hata hivyo Rais wa shirikisho la Filamu Rajab Amiri amesema sambamba na hilo imepelekea kukutana na marais wengine wa shirikisho,hivyo itapelekea kufungua milango mingine katika filamu haswa kwa waigizaji nchi hivyo wajiandae kupata matunda mazuri.

Alitoa rai kwa Tanzania tuendelee kushirikiana sisi kwa sisi na kujiaminisha kama tunaweza na huko tunapokwenda ni kwa ajiri yetu

Kwa upande wake Afisa filamu Ally  Makata  aliongezea lengo kubwa kama bodi ya filamu ni kuhakikisha wanaleta maendelea katika tathnia ya filamu na michezo ya kuigiza 

"Ikumbukwe kuwa michezo ya kuigiza na filamu imekuwa biashara na ajira kwa watu wengi hivyo ikatufanya tushiriki Mkutano huo ili kuwepo na makubaliano ambayo ni kujenga uwezo,na masoko yaliyozungumzwa ni yale ya ( Streem East) itakuwa app ambayo yenye lengo la kutengeneza kazi zenye ubora kwa wasanii ilikuweza kupata masoko nje na ndani ya Afrika" amesema Makata

Aidha mkutano huo ulihudhuriwa na nchi zaidi ya nane ambazo ni Tanzani,  Uganda, Kenya, Ethiopia, Malawi,Zambia, Rwanda.