Namna vijana wanavyonufaika kupitia teknolojia mpya ya mashine inayojiendesha yenyewe
Na Hawa Ismail
Amezungumza mkufunzi wa chuo cha veta kipawa ndugu Joshua Mwankusye leo 5 julai 2025 katika maonyesho ya 49 ya kimataifa ya biashara ametoa mafunzo yanayopatikana katika banda lake namna kijana anavyoweza kujiajiri kupitia mashine inayoweza kujiendesha yenyewe.
" Hii mashine inauwezo wa kupachika vizibo, kubandika lebo katika bidhaa hivyo husaidia kurahisisha kazi kupitia teknolojia hii ya kisasa" alisema Mwankusye
Aidha aliongezea kwa kusema unaweza kusomea teknolojia hii kwa muda wa miezi mitatu kwa ada ya shilingi 500000.


