RC CHALAMILA AWAALIKA WANANCHI MKOA WA DAR ES SALAAM KUPATA MSAADA WA KISHERIA KWA WALE WALIOUZIWA MAGARI MABOVU PAMOJA NA MIGOGORO YA ARIDHI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Albert Chalamila ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa kujitokeza kupata msaada wa kisheria katika ofisi za mkowa wa Dar es Salaam kuanzia juni 16 hadi 25 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam amesema kumekua na malalamiko mengi ya baadhi ya Wateja wa magari kwenye maeneo ya kuuzia magari kuuziwa magari mabovu.
"Hata kama lalamiko lako umelipeleka Mahakamani njoo na nyaraka zako ofisini kwangu kuna watalaamu wa kisheria watakusaidia , Alisema Challamila
Chalamila ameongeza kuw wale waliouziwa magari mabovu kwenye maeneo ya kuuzia magari pamoja na Wale wenye migogoro ya Ardhi wafike na nyaraka zao wapate msaada wa kisheria.
Kampeni Hii ya Mama Saimia imeanza kutekelezwa 2023 kwa pande zote za muungazo ambapo Zanzibar ni mikoa mitano na Bara ni mikoa ishirini.