ITRACOM WAIMARISHE MIFUMO YA USAMBAZAJI MBOLEA VIJIJINI
Na. Wellu Mtaki, Dodoma
Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewahimiza na kuomba kiwanda Cha mbolea Cha Itracom Kuimarisha mifumo ya usambazaji wa mbolea kwa wakulima waliopo vijijini .
Kauli hiyo ameitoa wakati wa Uzinduzi wa kiwanda Cha mbolea Cha Itracom Leo June 28 ,2025 Jijini Dodoma ambapo Mheshimiwa Rais alikuwa mgeni Rasmi akiwa sambamba na Rais wa Jamhuri ya Burundi Evarist Ndayishimiye.
Amesema licha ya kiwanda kufanya shughuri zake za kutengeneza mbolea bali watumie fursa ya kuwapa Elimu wa kulima juu ya umuhimu wa matumizi ya mbolea hizo kwani anaamini kiwanda hicho kinakaenda kukuza Sekta ya kilimo nchini.
"Nitoe rai kwa uongozi wa Kiwanda cha Itracom kuhakikisha kwamba mnaimarisha mfumo wa usambazaji wa mbolea hadi kwa wakulima waliopo vijijini ili waweze kuipata mbolea hii kwa gharama nafuu," amesema Rais Samia.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Nduwimana Naizaire ameipongeza hatua ya serikali ya Tanzania kuwapa moyo na kuwaunga mkono katika hatua zote za uwekezaji tangu mwaka 2020 walipoonesha nia hiyo.
Naizaire ameongeza kuwa pamoja na pongezi kwa Rais Samia suluhu Hassan pia amempongeza Rais wa Burundi Evarist Ndayishimiye kwa ushirikiano wake kwa mwekezaji wa kiwanda hicho.
sambamba na Hayo amesema kuwa kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha mbolea kiasi cha tani milioni moja jambo ambalo linawezesha wakulima kupata mbolea kwa uhakika na kubainisha kuwa katika kiwanda hicho ajira 1800 za moja kwa moja zimetengenezwa na ambazo sio za Moja kwa moja ni zaidi ya 3000 huku wakitarajia kupanda mpaka ajira elfu 15000.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi na Mtendaji mkuu wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela ameipongeza serikali kwa kuwezesha diplomasia ya uchumi kati ya kiwanda cha Itracom na CRDB huku akibainisha kuwa katika michakato ya uwekezaji huo Benki yao ilitoa kiasi cha Shilingi bilioni 215 katika kuunga mkono juhudi hizo za uwekezaji


