Breaking News

HALIMASHAURI YA JIJI LA DODOMA YAPATA HATI SAFI





Na. Wellu Mtaki, Dodoma 

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imepata hati safi ya ukaguzi na udhiti wa hesabu za serikali hali ambayo Jiji hilo linajivunia fahari pamoja na kujipanga vyema katika kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi.

Kauli hiyo imetolewa Leo na mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary senyamule wakati wa kikao cha Baraza la madiwani Jijini hapo mara baaada ya majadiliaono ya waheshimiwa madiwani pamoja na wataalamu akiwemo mkaguzi wa ndani wa Halmashauri Jijini hapo 

Amesema hoja zote za ukaguzi mkuu wa hesabu za serikali  pamoja na zile za ndani zitekelezwe  ipasavyo ili ziweze kuhakikiwa  na kufungwa kwa kuzingatia Sheria kanuni na taratibu za serikali 

" Hati hii imeipa heshima mkoa wa Dodoma tangu mwaka 2017 ,2018 hadi Sasa Mkoa huu umepata hati safi na wataendelee kuhakikisha tunapata hati safi Kila mwaka" amesema Senyamule.

Aidha ameelezea kuwa mkoa wa Dodoma umebainika kuwa na uwezo wa kulima zao la Apple, kwa  mujibu wa utafiti uliofanywa na wataalamu wa kilimo wamebaini aina mbili ya miche zinazoweza kuota kwenye mkoa huo na Sasa Mkoa huo umeanza kulima zao hilo.

Kwa upande wake  mstahimiki meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis mwafupe amewaasa madiwani wa mkoa huko kuwa mfano bora katika Jamii zao na kuhakikisha wanawajibika ipasavyo Katika kata Zao kwa kufuata Sheria na taratibu za Nchi hasa Katika kipindi hiki Cha kuelekea uchanguzi.
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma huwa linautaratibu wa kukutana kwa ajili ya kujadili taarifa ya udhibiti wa hesabu za serikali ambapo hoja 86 ya repoti ya mkaguzi mkuu wa serikali zimejadiliwa ikiwa hoja 45 ni za miaka ya nyuma.