ATAKAYEUZA MAFUTA YA PETROLI ZAIDA YA BEI SHILLING 2905 ATAFUKIWA KITUO.
Wellu Mtaki, Dodoma .
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA) imewataka wauzaji wa Vituo vya petroli kufuata taratibu na Sheria iliyopangwa na Mamlaka kwani bei ya mafuta ni shilling 2905 lakini baadhi Vituo wanauza mafuta kwa Bei ya shilingi 5000 huku akisisitiza kwa yoyote atakayethibitika atachukuliwa hatua Kali ikiwemo kufungiwa kituo chake.
Kauli hiyo ameitoa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt.James Andilile wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Amesema kwa yoyote atakayekubwa na madhara hayo wapinge simu ya bure 0800110030 ili kutoa taarifa maana huo ni ukiukwaji wa sheria .
Aidha ameeleza kuwa Mamlaka inaendelea kuboresha mifumo ya utoaji huduma ambapo kwa Sasa waombaji wa leseni hawahitaji kufika ofisini ili kupata huduma bali huduma zote zinapatikana kwenye mitandao yao ya kidigitali .
Amesema kama sehemu ya kuchochea uwajibikaji kwa taasisi wanazosimamia ,wamezitaka kuingia mikataba ya huduma kwa wateja na kwa sababu mara nyingi unaweza kukuta watoaji wa huduma hawatoi taarifa kwa wakati,wamewaelekeza kuhakikisha kwamba wanaweka taarifa kwenye website zao kama mikataba ya huduma kwa wateja
EWURA ni moja kati ya Mamlaka za Serikali zinazoshiriki maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma 2025 ikiwa ni sehemu ya taasisi za Serikali zinazolenga kuboresha huduma wanazozitoa kwa wateja wao.
