WAZAZI WAHIMIZWA KUWAPELEKA WATOTO WENYE ULEMAVU KATIKA SHULE ZA BINAFSI
Mwandishi wetu Dodoma
MKURUGENZI Mtendaji wa shule ya awali na msingi ya New Precious Michese Dodoma Justina Mhoja,amewataka wazazi na walezi,wenye watoto ambao wana mahitaji maalumu kuwapeleka kwenye shule za watu binafsi badala ya kuwa na hofu ya kukataliwa.
Mhoja ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma,wakati akiwasisitizia wazazi na walezi wenye watoto ambao wana ulemavu kuwapeleka kwenye shule hizo badala ya kuwa na hofu ukizingatia kuwa miundombinu ya majengo ni rafiki pia.
Alisema kuwa hakuna sababu ya kuwafungia majumbani watoto hao wenye mahitaji maalum kutokana na hofu ya kukataliwa,kwa kuwa haki ya kupata elimu wanayo bila kuangalia kama ni shule za serikali au watu binafsi.
"Naomba niwasii wazazi wenye watoto ambao wana mahitaji maalum wasiwe na hofu ya kuwapeleka kwenye shule hizo za watu binafsi,badala yake wawapeleke ukizingatia kuwa hivi sasa majengo yameboreshwa kuanzia miundombinu hadi vitabu vya kusom"alisema.
Hivyo hakuna sababu ya familia zenye watoto ambao wana ulemavu kuwaweka majumbani watoto mwenye ulemavu,majengo ya shule hivi yameboreshwa na wanaweza kupata mahitaji yote yanayokatakiwa kama ilivyo kwa wengine wasiokuwa na ulemavu.
Naye Mwalimu mkuu wa shule ya awali na msingi wa New Precious Michese ameishukuru serikali kwa kuzindua mtaala mpya ulioboreshwa wa elimu ambao hivi sasa utawaweza wanafunzi kuwasaidia kupata ujuzi wakiwa bado wapo mashuleni.
Alisema kuwa kuwepo kwa mtaala huo ulioboreshwa utawawezesha wanafunzi mashuleni kujifunza masombo mbalimbali kwa vitendo kuanzia ngazi ya chini na hatimaye watakapomaliza wataweza kupata ujuzi na kupata ajira.
"Hivyo sisi kama shule binafsi tunaishukuru serikali kwa kuzunduliwa kwa mtaala huo ulioboreshwa,na tunaamini watoto wetu sasa wataweza kujifunza ujuzi ambao wakija kumaliza masomo wataweza kujipatia ajira kutokana na kile walichojifunza darasani"alisema
Shinyanga hata hivyo amewaomba wazazi kutoa ushirikiano katika kununua mahitaji ya watoto ikiwemo vitabu,ili kuwaboreshea masomo wanayojifunza,badfala ya kuiachia serikali peke na wadau mbalimbali wa elimu.

