Breaking News

WATU MILIONI 600 AFRIKA HAWAJAFIKIWA NA UMEME; TUTUMIE RASILIMALI ZILIZOPO KUBADILISHA MAISHA - DKT. BITEKO


Na Mwandishi wetu Arusha

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,  Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Bara la Afrika lina zaidi ya watu milioni 600 ambao bado hawajafikiwa na nishati ya umeme hivyo rasilimali zilizopo zitumike kubadilisha maisha ya watu ikiwemo katika sekta ya umeme.

Dkt. Biteko ameyasema hayo Desemba 04, 2024 wakati akifunga Mkutano wa Pili wa Mwaka wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa Nchi za Afrika (AAAG) Jijini Arusha.

Amesisitiza  rasilimali zilizopo barani Afrika zitumike kubadilisha hali za maisha ya watu ili ziweze kuleta tija.