Breaking News

CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI NIT KIMEWAPA TUZO WAHITIMU 4176

 




Na Angelina Mganga,DmNewsOnline

DAR ES SALAAM 

MKUU wa Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji Mhandis Dkt.Prosper Mgaya amesema jumla ya wahitimu 4176 wametunukiwa tuzo mbalimbali ambapo wanawake ni 1595 sawa na asilimia 38.

Amesema hayo katika mahafali ya arobaini ya chuo hicho kuwa watahakikisha idadi ya wanafunzi wa kike inaongezeka kwenye taaluma za uchukuzi na usafirishaji kwa kuweka mpango mkakati wa miaka mitano wa chuo kwa kuhamasisha katika shule za sekondari.

Aidha amewataka wahitimu wakafanye kazi kwa ufasaha,kujituma,ubunifu,nidhamu na uadilifu

Kwa upande wake Mgeni rasmi Naib Waziri wa Uchukuzi,David Kihenzile  amesema  amefarijika kuona idadi ya wahitimu kuongezeka katika maeneo ya kimkakat i(Usafiri wa Reli,Usafiri wa Maji na Usafiri wa Anga.Idadi hii ya wahitimu ni ushahidi tosha wa juhudi kubwa ya chuo kuhakikisha kuwa na wataalam wa kutosha katika Sekta ya Uchukuzi.


Naibu Waziri wa Uchukuzi ametoa wito kwa uongozi wa chuo kuendelea kuwa wabunifu na kufanya kazi Kwa bidii ili kukifsnya chuo kuendelea kuwa mahali sahihi kwa ajili ya kuandaa wataalamu katika Sekta hii.


Aidha amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuwekeza katika sekta ya Uchukuzi hasa katika Ujenzi wa Barabara na madaraja,ujenzi wa RELI ya kisasa(Dar-Dom imekamilika na inatoa huduma,Dodoma Hadi Mwanza ujenzi unaendelea,Tabora-Kigoma ujenzi unaendelea,ujenzi na ukarabati wa Meli(Ziwa Tanganyika,Ziwa Victoria),Ujenzi na upanuzi wa bandari (Dar es Salaam,Mtwara-Kisiwa Mgao,Bukoba,Mwanza,Ziwa Nyasa-Mbambay) Ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege (Musoma,Mwanza,Bukoba,Shinyqnga,Tabora Rukwa,Mtwara,Lindi na Ununuzi wa ndege kwani uwekezaji huu unahita wataalama watakaoendesha na kusimamia kwa ustadi miradi hii ili kukuza uchumi wa nchi.

Pia amekitaka chuokutoa  elimu Bora na kuandaa wataalam wakutosha katika sekta ya Uchukuzi na Usafirishaji pia amewaahidi kuwa serikali itaendelea kukiwezesha chuo ili kuhakikisha kuwa kinatimiza majukumu yake ya kuandaa wataalam,kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalam katika sekta ya uchukuzi kwa maendeleo ya Taifa.

"Chuo kipo katika hatua za mwisho za kukamilika ujenzi wa baadhi ya  hmiundombinu hiyo kupitia Mradi wa EASTRIP unaofdhiliwa na Benki ya Dunia ikiwemo mabweni yamekamilika kwa asilimia 97",amesema

Alimalizia kwa kusema kwamba Serikali kwa kushirikiana na NIT iko katika hatus za kusndaa mapendekezo ya kutunga Sheria ya Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Uchukuzi.Lengo la Bodi kuwatambua,kuwasajili  na kusimamia weledi na maadili ya wataalam wa Uchukuzi Tanzania Bara ili kuhakikisha kwamba kazi zote za usafirishaji zinasimamiws na watu wenye taaluma stahiki.