NMB, ORBIT ZANG'ARA TUZO ZA DSE 2024
KAMPUNI ya ORBIT Securities nchini imepongeza mchakato wa utoaji tuzo kwa wanachama wa Soko la Hisa la Dar es Salam (DSE), kwamba utachagiza juhudi sambamba na kuhamasisha elimu ya uwekezaji kwenye masoko ya mitaji bienkwa azma chanya ya kukuza uchumi
Hafla ya tuzo hizo ambazo kwa mwaka huu zimeratibiwa na Benki ya 'Mwanga Hakika' kwa kushirikiana na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) zimefanikisha utoaji wa tuzo za wanachama wa DSE kwa mwaka 2024, zikihusisha makampuni, mabenki, na viwanda vilivyokidhi vigezo vya utendaji bora.
Akizungumza muda mfupi baada ya kumalizika kwa utoaji wa tuzo hizo Dar es Salaam hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Godfrey Gabriel alisema tuzo hizo zitaongeza chachu kwa jamii kuanza kujikita kwenye masuala ya mitaji.
"Ni tuzo zinazotoa hamasa kubwa ya jamii kusonga mbele kwenye uwekezaji wa mitaji; mathalani, kampuni yetu (orbit) imejinyakulia tuzo mbili, ikiwemo tuzo ya 'Best Broker of the Year 2024,' kutokana na juhudi zake katika ustawi wa mazingira, masuala ya kijamii, na utawala (ESG)," alisema.
Aidha, Mkuu wa Idara ya Uhusiano kwa wawekezaji Benki ya NMB, Innocent Yonazi amefurahishwa na tuzo hizo, ambapo wao kama benki walipata tuzo nne.




