Breaking News

WAZIRI CHANA : TAWIRI NI MOYO WA UHIFADHI WA WANYAMAPORI NCHINI





Na Mwandishi Wetu, Arusha

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana(Mb) amesema Serikali imekuwa ikitumia  takwimu za kisayansi kufanya maamuzi yaliyojikita kuimarisha uhifadhi wa Wanyamapori ili kuwa na  Utalii endelevu

Mhe.Chana ametoa kauli hiyo leo Oktoba 16,2024  Jijini Arusha wakati akizungumza na Menejimenti yaTaasisi  ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Njiro - Arusha ambapo amesema Taasisi hiyo ni muhimu  kwa uhifadhi nchini.

" Tunahakikisha rasilimali hii ya Wanyamapori ipo kwa kizazi cha leo na kijacho ambapo  matumizi ya takwimu za kisayansi ni dira katika uhifadhi  amesisitiza Waziri Chana.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Dkt.Eblate Mjingo amesema takwimu za tafiti zinasaidia kunadi Utalii ikiwa ni pamoja na kuelekeza  namna bora ya kufanya Utalii sambamba na kuimarisha uhifadhi

Kikao hicho kimehudhuriwa  na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utalii, Nkoba Mabula, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Dkt.  Thereza Mugobi, wawakilishi kutoka Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii na Maafisa Waandamizi kutoka TAWIRI.