Breaking News

SERIKALI YAONGEZA NGUVU KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI KUPITIA MIKOPO, TAFITI NA TEKNOLOJIA ILI KUKUZA AJIRA NA UCHUMI WA TAIFA.


Na Mwandishi wetu, Dar es salaam 

Serikali imeeleza dhamira yake ya kuifanya sekta ya madini kuwa injini ya ukuaji wa uchumi, ajira na mapambano dhidi ya umasikini kupitia uwezeshaji wa wachimbaji wadogo nchini.

Akizindua ripoti ya mapendekezo ya kuendeleza wachimbaji wadogo wa madini, Profesa Kitila Mkumbo alisema serikali itaendelea kuimarisha tafiti za madini na kuongeza ushiriki wa Watanzania katika kunufaika na rasilimali za taifa.

Naye Waziri wa Madini Anthony Mavunde alisema serikali imeanza kuweka mifumo ya mikopo, maeneo rasmi ya uchimbaji na matumizi ya teknolojia ili kuongeza tija kwa wachimbaji wadogo na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara ya madini barani Afrika.